Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 28, 2015

MATUMLA ALIVYOMCHAKAZA MCHNA WANG DIAMOND JUBILEE


. Bondia Mohammed Matumla akiwa amenyanyuliwa mkono  na mwamuzi Emanuel Mlundwa  baada ya kumchapa kwa pointi bondia Wang Xing Hua kutoka China kwenye pambano la raundi kumi lililofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam


Bondia Mohammed Matumla (kushoto) akimrushia makonde bondia Wang Xing Hua kutoka China kwenye pambano la raundi kumi lililofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo Matumla alishinda kwa pointi.

BONDIA Mohammed Matumla amewapa raha Watanzania baada ya kumchapa kwa pointi bondia Wang Xing Hua kutoka China kwenye pambano lililofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Matumla ambaye alikuwa akinolewa na baba yake mzazi, Rashid Matumla 'Snake Man' alionyesha kiwango cha juu kwani pambano lilikuwa la vuta nikuvute hadi akafanikiwa kumshinda Mchina huyo.

Katika pambano hilo Matumla haikuwa kazi rahisi kwa mtoto huyo wa Matumla kutokana na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na raia huyo wa China kwenye pambano hilo la raundi kumi

Matumla alifanya kazi kubwa naya ziada kumshinda Xiang ambaye alionyesha kiwango kizuri hadi kufanikiwa kupata ushindi wa pointi  kwani Mchina huyo, aliwapa hofu Watanzania waliokuwa ukumbini hapo kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha.

Hata hivyo ilipofika raundi ya nane, baadhi ya Wachina waliokuwa katika ukumbi huo walianza kuondoka wakiamini ndugu yao asingeshinda pambano hilo.

Katika pambano lingine la utangulizi bondia Mada Maugo amemaliza ubishi kwa kumtwanga Japhet Kaseba kwa KO.
Maugo amemchapa Kaseba katika raundi ya nane  na kuzima tambo za Kaseba baada ya kumchapa konde lililompeleka chini na kushindwa kuinuka na mwamuzi akalazimika kumaliza pambano.

Katika pambano jingine, Karama Nyilawila alimshinda Ibrahim Tambwe kwa KO katika raundi ya pili na Ashraf  akammaliza Ally Ramadhani kwa KO katika raundi ya pili tu.

No comments:

Post a Comment