Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 12, 2015

IRINGA KIBIKI CHILDREN CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI IRINGA

MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI
Mratibu wa KIBIKI CUP Haruna Saleh akiwa na FRANK KIBIKI



LIGI inayoshirikisha watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho kutwa kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.

Ligi hiyo  ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa na  inajulikana kama  Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino).

Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema  lengo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.

“Lengo ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu wenyewe ulemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema.

Pia alisema mpira ni ajira na huu hauna dini, kabila wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumeanzisha ligi ili kuendelea kukuza vipaji lakini tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alisema ligi hiyo imepata bara za shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa, ambalo watoto wameshafundishwa mafunzo ya waamuzi ambao ndio watakaochezesha ligi hiyo

No comments:

Post a Comment