Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 12, 2015

KILUVYA, MBAO FC, MJI NJOMBE, MJI MKUU ZAPANDA FDL

Timu za Kiluvya United ya Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza, Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza katika misimamo ya makundi yao ya Ligi Daraja la Pili (SDL).
Kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (8) ya Ligi Daraja 9SDL Toleo la 2014, hatua ya pili Ligi Daraja la Pili kutafuta Bingwa na sasa timu hizo zitacheza kusaka Bingwa wa ligi Daraja la Pili.
Mji Njombe itacheza na timu ya Kiluvya United tarehe 14 Machi mwaka huu katika uwanja wa Amani Makambako, na mchezo wa marudiano kufanyika tarehe 18 Machi, 2015 katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Nayo Mbao FC ya Mwanza watawakaribisha timu ya Mji Mkuu FC mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na mechi ya marudiano itachezwa Machi 18, 2015 katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Fainali inatarajiwa kufanyika Machi 22 mwaka huu jijin Dar es salaam (uwanja wa mchezo utatangazwa baadae) kwa kuzikutanisha timu zilizopata pointi nyingi katika michezo hiyo miwili ya awali.

No comments:

Post a Comment