Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 2, 2015

IBRAHIM CLASS 'KING CLASS MAWE' BINGWA WA U.B.O AFRIKA BAADA YA KUMPIGA COSMAS CHEKA KWA POINTI


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Afrika  uliofanyika jumamosi uwanja wa ndani wa Taifa. Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Pointi na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Afrika wa W.P.B.F na U.B.O Africa


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Afrika uliofanyika juzi.

Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Afrika

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya mpambano wake na Cosmas Cheka

BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Afrika kwa kumpinga bondia Cosmas Cheka wa Morogoro kwa pointi katika pambano la raundi kumi lililofanyika katika Uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Pambano lilianza kwa mashambilizi ya kushtukiza huku kila bondia akimtupia makonde mwenzie jambo lililofanya kuwa wa vuta nikuvute kwa kila mmoja kwani  walijiandaa kwa muda mrefu lakini mwishowe Class akaibuka kidedea baada ya raundi kumi kumalizika
Akizungumza baada ya pambano hilo bondia, Ibrahim Class alisema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kushinda pambano hilo kwani mpinzani wake naye alikuwa mzuri.
“Cheka siyo bondia wa kumfanyia masihara kama sikujiandaa vizuri angeweza kunipiga kwani ngumi zake nzito lakini namshukuru Mungu nimeshinda”, alisema Class.

Katika mapambano mingine iliyopigwa bondia Fadhili Majiha alimpiga Francis Miyeyusho kwa pointi huku Vicent Mbilinyi  na Epson John wa Morogoro kumaliza kwa sare.
Bondia Shedrack Ignas alimpiga bondia Husein Mbonde kwa KO ya raundi ya nne ya pambano naye Saidi Mundi akimpiga kwa pointi bondia Ramadhani Shauri

Mashabiki waliofika kuona pambano huo wameomba mapambano yawe yanaanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafiri wakati wa kurudi kwenda majumbani kwani wengi wanategemea usafiri wa daladala


No comments:

Post a Comment