Kocha Tim Sherwood akishangilia.
Aston Villa imetinga Nusu Fainali ya FA CUP baada ya Jana kuwachapa West Bromwich Albion Bao 2-0 Uwanjani Villa Park.
Bao za Villa kwenye Dabi hii ya Midlands zilifungwa Kipindi cha Pili na Fabian Delph na Scott Sinclair.
WBA walimaliza Mechi hii wakwa Mtu 10 baada ya Claudio Yacob kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.
Mechi hii ilishuhudia Mashabiki wakivamia Uwanja kabla Filimbi ya mwisho kupigwa na ililazimika watelowe ili Mechi iendelee.
Katika Mechi nyingine ya Robo Fainali, Bradford na Reading zilitoka 0-0.
Fabian Delph akishangilia bao lake baada ya kufanya 1-0 dhidi ya West Brom Albion


VIKOSI:
Aston Villa: Given, Bacuna, Okore, Clark, Lowton, Cleverley, Westwood, Delph, N'Zogbia, Agbonlahor, Sinclair.
Akiba: Guzan, Weimann, Sanchez, Gil, Kinsella, Calder, Grealish.
West Brom: Myhill, McAuley, Dawson, Olsson, Lescott, Yacob, Morrison, Berahino, Gardner, Brunt, Ideye.
Akiba: Foster, Wisdom, Baird, Pocognoli, McManaman, Mulumbu, Sessegnon.
Refa: Anthony Taylor

No comments:
Post a Comment