Yanga |
YANGA inaleta heshima kwa Watanzania. Yanga tamu mwe! Hayo
yote unaweza kuyatumia kutamka ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Yanga jana dhidi
ya BDF XI kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa hatua ya awali katika michuano ya Kombe la
Shirikisho umeiweka Yanga katika nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele katika
mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo mjini Gaborone, Botswana, ambapo Yanga
sasa itahitaji ushindi ama sare
ya aina yoyote au isifungwe zaidi ya bao 1-0 ili isonge mbele.
Yanga ilianza
kuhesabu bao dakika ya kwanza, mfungaji akiwa Mrundi Amis Tambwe kwa kichwa
kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Dakika 20 za mwanzo
BDF XI inayomilikiwa na Jeshi la Botswana, ilionekana kuzidiwa na wachezaji wa
timu hiyo kujilinda zaidi badala ya kushambulia, hali iliyowapa mwanya Yanga
kupanga mashambulizi.
Kipindi cha pili
kilianza kwa Yanga kushambulia kwa kasi, huku BDF XI wakionekana kupoteza muda
zaidi kwa kuhitaji matokeo yabaki kama yalivyo.
Lakini dakika ya 56
Tambwe alifunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa, bao
ambalo lilionekana kuwachanganya wachezaji wa BDF XI.
Dakika ya 64, 65 na
67 lango la BDF XI lilikuwa katika hekaheka, lakini Nadir Haroub, Andrey
Coutinho na Haruna Niyonzima kwa nyakati tofauti walishindwa kutumbukiza mpira
wavuni.
Yanga: Ally
Mustapha, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Salum
Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe/Jerry Tegete, Mrisho
Ngassa na Andrey Coutinho/Kpah Sherman
No comments:
Post a Comment