Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 24, 2015

WAYNE ROONEY ASEMA NI MUHIMU KUIFUNGA SUNDERLAND JUMAMOSI ILI WACHEZE KLABU BINGWA ULAYA


NAHODHA wa Manchester United ametamka kuwa baada ya kufungwa na Swansea City basi hawana budi kuifunga Sunderland Jumamosi la sivyo wataikosa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Jumamosi, wakicheza huko Liberty Stadium, Man United waliongoza Bao 1-0 lakini wakairuhusu Swansea kuwachapa Bao 2-1 kikiwa ni kipigo chao cha pili katika Mechi 20 zilizopita chini ya Meneja Louis van Gaal.
Ingawa bado zipo Mechi 12 hadi Msimu wa Ligi Kuu England kunamalizika, lakini Mechi zao 7 baada ya Sunderland Jumamosi hii ni dhidi ya Tottenham na Liverpool, zinazowania 4 Bora kama wao, pia dhidi ya Manchester City na Chelsea ambazo ndizo ziko kwenye mbio za Ubingwa Msimu huu na pia dhidi ya Everton inayozidi kuimarika baada ya kuyumba.
Hali hiyo imemfanya Kepteni Wayne Rooney kupiga Mbiu ya Mgambo kwamba ushindi Jumamosi hii inayokuja dhidi ya Sunderland Uwanjani Old Trafford ni kitu cha lazima.
Kepteni Rooney ametamka: “Tunahitaji kulipa Mechi ijayo. Ni Gemu ambayo ushindi ni lazima. Tunatakiwa kushinda ili turudi kwenye reli na kuanza mbio nyingine za ushindi tumalize 4 Bora!”
Luis Van Gaal akitoka Uwanjani baada ya kubamizwa bao 2-1 na Swansea City Wachezaji wa Swansea City wakishangilia baada ya kuibamiza United  hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment