Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 27, 2015

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA MWAMUZI MOHAMED NYAMA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya Bw. Nyama, kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu Mohamed Nyama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi  ya TFF kilichotokea jana kwao Nachingwea- Lindi.
Marehemu Mohamed Nyama wakati wa uhai wake alikuwa mwamuzi wa daraja la kwanza ambaye pia alitambuliwa na FIFA, Nyama anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwao Nachingwea mkoani Lindi na TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Athumani Kambi.
Katika salam zake kwa familia ya Nyama, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini  katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

No comments:

Post a Comment