Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 11, 2015

LESENI KWA VILABU KUANZA KUTOLEWA KABLA YA MSIMU

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi jana Jumapili tarehe 08 Februari, 2015 katika kikao chake cha kawaida.  Pamoja na kujadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 na 15 mjini Singida, Kamati ilijadili na kuamua yafuatayo:-

1.   Zoezi la utoaji leseni kwa vilabu litaanza kabla ya msimu wa ligi 2015/16.  Vilabu vitatumiwa fomu za maombi mapema iwezekanavyo ili viweke nyumba zao sawa na kuleta maombi.  Leseni za vilabu (club licence) ni agizo la CAF na FIFA katika kuhakikisha vilabu vinaendeshwa kwa weredi.  Baadhi ya maeneo yanayoagaliwa katika utoaji wa leseni ni pamoja na kuwepo kwa Sekretarieti, miundo mbinu ya mazoezi na mashindano, hadhi za kisheria (legal status) mikataba ya ajira n.k.

2.   Kamati ya Utendaji imeazimia kufanyika kwa mashindano ya Taifa Cup kwa upande wa wanaume.  Sekretarieti ya TFF imetakiwa kufanya juhudi ili mashindao hayo yaweze kufanyika.

3.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetoa pongezi kwa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa juhudi zake za kukuza soka la vijana kupitia mradi wake wa kuanzisha shule ya soka (Academy) kwa ushirikiano na klabu ya Real Madrid ya Hispania.  Aidha Kamati ya Utendaji ya TFF imeipongeza Kampuni ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa juhudi zao za kuchangia maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu kwa ujumla ikiwa ni kupitia mpango wa kujenga shule ya soka (academy) uwezeshaji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 13 (U-13) yatakayofanyika mwezi April, 2015 mjini Mwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya soka na michezo kwa ujumla.

Kamati ya Utendaji imewaomba wadau wengine kufuata mifano hiyo na kuchangia maendeleo ya soka kwani kazi hii inategemeana ni kwa faida ya wadau mbali mbali.

4.   Kamati ya Utendaji ilipokea mabadiliko ya uwakilishi wa Chama cha Soka la Wanawake nchini (TWFA) yaliyotokana na kuondoka kwa Bi. Lina Kessy aliyekuwa Mwenyekiti wake.  Bi. Lina ameajiriwa kama Afisa michezo wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.  Nafasi ya Mwenyekiti inachukuliwa na Bi. Rose Kisiwa ambaye hapo kabla alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TWFA ataendelea kuwa Mwenyekiti mpaka hapo utakapokaa Mkutano Mkuu wa kawaida wa TWFA.

5.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo kwa vitendo vya vurugu na utovu wa nidhamu katika mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini.  TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu hususani viongozi wa vilabu kutilia mkazo elimu ya kujitambua ili wachezaji wajue kuwa wao ni hazina ya Taifa na kioo (taswira) cha jamii, hivyo waepuke vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.  Vitendo hivi si tu vinakwamisha maendeleo, bali pia vinawadharirisha wao, mpira wa miguu na jamii kwa ujumla.

Kufuatia matukio ya hivi karibuni na kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu kwa haraka na weredi, Kamati ya Utendaji imeteua ya Kamati ya kuangalia na kusimamia kanuni za uendeshaji Ligi. Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Bodi ya Ligi, Kurugenzi ya mashindano, Kamati ya mashindano na kamati ya waamuzi.

No comments:

Post a Comment