Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa
Squad, Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao
haukufuata kanuni za usajili.
Villa
Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala
ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad
ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki
ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko
ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad
kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni
mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita
mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili
majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala
la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi
thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of
doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda
ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu
hiyo.
JKT
MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu
ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada
ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu
kwenye mechi.
Uamuzi
huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza
malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa
sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.
Kamati
imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi
yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo
ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale
imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia
malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi
yake ya mwisho ya ligi.
No comments:
Post a Comment