Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto kuwa
Ofisa Habari kuanzia Februari 1 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo,
Kizuguto alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga nafasi aliyoitumikia kwa miaka
miwili.
Kizuguto ana
Stashahada ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha Learn IT cha Dar es Salaam. Pia, ana ujuzi wa
kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta na uchambuzi wa mifumo ya kompyuta.
Mei mwaka jana,
Kizuguto aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kuhudhuria
mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao
(TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.
Akizungumza baada ya
kutangazwa na Katibu Mkuu Mwesigwa Baregu Kizuguto aliahidi kutoa ushirikiano
kwa waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment