Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 16, 2015

RATIBA AFCON 2015: KUANZA KESHO EQUATORIAL GUINEA vs CONGO.

MASHINDANO ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, yanaanza Nchini Equatorial Guinea Jumamosi Januari 17 na Nchi 16, wakiwemo Wenyeji, watachuana kwa kuanzia Mechi za Makundi.
Yapo Makundi Manne ya Timu 4 kila mmoja na Timu mbiliza juu toka kila Kundi zitaingia Robo Fainali.
Mechi za Makundi zitachezwa katika Miji ya Bata, Malabo, Mongomo na Ebebitin.


VIWANJA:
-Estadio de Bata, Mjini Bata, Watazamaji 37,500
-Nuevo Estadio de Malabo, Malabo, Watazamaji 15,250
-Estadio de Mongomo, Mongomo, Watazamaji 10,000
-Nuevo Estadio de Ebebiyín, Ebebitin, Watazamaji 5,000

Jumamosi zitakuwepo Mechi mbili za ufunguzi za Kundi A na ya kwanza ni ya Wenyeji Equatorial Guinea watakapocheza na Congo ndani ya Estadio de Bata Mjini Bata na kufuatia Mechi ya Burkina Faso na Gabon Uwanjani hapo hapo.

Kila Siku kutakuwa na Mechi mbili na Fainali ya Mashindano haya itachezwa Februari 8, Estadio de Bata, Mjini Bata.

Awali Mashindano haya yalikuwa yachezwe Nchini Morocco lakini Nchi hiyo ilijitoa kwa kuhofia Ugonjwa wa Ebola uliolipuka huko Afrika Magharibi na CAF kuipa Uenyeji Equatorial Guinea Nchi ambayo Mwaka 2012 iliweza pia kuwa Mwenyeji wa Mashindano haya pamoja na Gabon ambapo Zambia waliibuka Mabingwa.
AFCON 2015:RATIBA
Jumamosi Januari 17

19:00 Equatorial Guinea v Congo [Estadio de Bata]
22:00 Burkina Faso v Gabon [Estadio de Bata]

Jumapili Januari 18
1900 Zambia v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
2200 Tunisia v Cape Verde Islands [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumatatu Januari 19
1900 Ghana v Senegal [Estadio de Mongomo]
2200 Algeria v South Africa [Estadio de Mongomo]

Jumanne Januari 20
1900 Côte d'Ivoire v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]
2200 Mali v Cameroon [Nuevo Estadio de Malabo]

Jumatano Januari 21
1900 Equatorial Guinea v Burkina Faso [Estadio de Bata]
2200 Gabon v Congo [Estadio de Bata]

Alhamisi Januari 22
1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Ijumaa Januari 23
19:00 Ghana v Algeria [Estadio de Mongomo]
22:00 South Africa v Senegal [Estadio de Mongomo]

Jumamosi Januari 24
1900 Côte d'Ivoire v Mali [Nuevo Estadio de Malabo]
2200 Cameroon v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]

Jumapili Januari 25
21:00 Gabon v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]
21:00 Congo v Burkina Faso [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumatatu Januari 26
21:00 Congo DR v Tunisia [Estadio de Bata]
21:00 Cape Verde Islands v Zambia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumanne Januari 27
21:00 South Africa v Ghana [Estadio de Mongomo]
21:00 Senegal v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]

Jumatano Januari 28
21:00 Cameroon v Côte d'Ivoire [Nuevo Estadio de Malabo]
21:00 Guinea v Mali [Estadio de Mongomo]

ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 31

19:00 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Estadio de Bata]==RF1
22:00 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nuevo Estadio de Ebebiyín]==RF2

Jumapili Februari 1
19:00 Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Estadio de Mongomo]==RF3
22:00 Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Nuevo Estadio de Malabo]==RF4
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 4

22:00 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]==NF1

Alhamisi Februari 5
22:00 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]==NF2

MSHINDI WA 3
Jumamosi Februari 7

21:00 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]

FAINALI
Jumapili Februari 8

22:00 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]

No comments:

Post a Comment