Na Faustine Ruta, Mwanza
Timu ya Wanawake kutoka Mkoa wa Kagera imetupwa nje ya Mashindano hayo leo kwenye Matuta baada ya kumaliza mtanange wao kwa sare ya Nyumbani Ushindi wa 2-1 na leo Ugenini CCM Kirumba Mwanza 2-1 na Matuta kupigwa na Timu ya Mwanza kuibuka na Ushindi wa bao 4-3. Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Timu ya Mwanza ndio walianza kupata bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa mchezaji wao matata aliyekuwa amevaa jezi no.10 Meriam Kimbuya kwa kukatika katikati ya mabeki na kufunga bao hilo la kwanza. Kipindi cha pili mchezaji huyo huyo Meriam Kimbuya aliwafungia bao tena Mwanza katika dakika ya 64 na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Kagera. Kagera waliongeza Bidii nao dakika ya 73 Mchezaji Anna Katunzi aliachia shuti kali lililomzidi nguvu kipa wa Mwanza na kuishilia nyavuni na kufanya 2-1.

Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Hapa jijini Mwanza wakishangilia baada ya kuifunga Timu ya Kagera kwa matuta. Mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo Mchana kwenye raundi ya hatua ya 16 Bora.
Raha ya Ushindi!!
Mchezaji wa Timu ya Mwanza Meriam Kimbuya akishangilia bao lake la dakika ya 2

Kikosi cha Timu ya Kagera kilichoanza.
No comments:
Post a Comment