Kikosi cha Polisi Mara wakifanya mazoezi Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya
Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake
za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa
vinginevyo.
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu
wa amani ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye
uwanja huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga
ambapo waamuzi walipigwa.
Kamati zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio
yote ya utovu wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika
ikiwemo na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa
kutosha viwanjani wakati wa mechi.
No comments:
Post a Comment