SHIRIKISHO
la Soka Tanzania(TFF) limemteua mchezaji wa zamani wa Yanga John Mwansansu kuwa
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni, akisaidiana na Ally Sharif wa
Zanzibar.
Akitangaza
uteuzi huo jana Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni wa TFF Ahmed Mgoi alisema Mwansansu na msaidizi wake huyo watakuwa na kazi ya
kuchagua wachezaji wa timu ya taifa wa soka la ufukweni ambao watajiandaa na
michuano ya Afrika.
Kwa mujibu
wa Mgoi, fainali za michuano ya Afrika
ya mchezo huo yatarajiwa kufanyika April Mwaka huu Sheli sheli.
Alisema ili
Tanzania iweze kufunzu imepangwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kenya
utakaochezwa nchini humo kati ya Februari
13 na 15 kisha kucheza mchezo wa marudiano Dar es Salaam kati ya Februari 20,
21 na 22.
“Tanzania tutashiriki mashindano hayo kwa mara ya
kwanza, hivyo baada ya kumpata Kocha tutaanza maandalizi ya kusaka nafasi hiyo,
tushiriki kwenye fainali za Afrika,”alisema.
Mgoi alisema
kikosi cha timu ya Taifa kitaundwa na wachezaji waliofanya vizuri kwenye
mashindano ya vyuo vikuu yaliyofanyika Zanzibar mwaka jana, ambapo watatajwa
hivi karibuni kisha kuingia kambini.
Alisema
wachezaji wa Zanzibar na Tanzania Bara wataungana katika kambi ya pamoja na
kucheza michezo ya kirafiki ambapo baadaye watachaguliwa wachezaji watakounda
timu ya taifa kwa ajili ya michuano hiyo.
“Kikosi
kitatangazwa na Mwansansu kuanzia Januari 19, mwaka huu, kwa upande wa Zanzibar tayari wanajulikana kwa vile
walianza muda mrefu na mazoezi ya pamoja na timu ya
Zanzibar yatafanyika Januari 24 na 25 mwaka huu,”alisema.
Alisema
iwapo watafanikiwa kuitoa Kenya kwenye hatua za awali, watakutana na Misri
ambapo wakifanya vizuri, watakuwa wamefuzu kushiriki fainali za michuano hiyo.
Kuhusu
viwanja vitakavyotumika, alisema atataja viwanja vinne baadaye ambapo
watawekeza, kwani ndio kwanza wanaandaa mkakati wa maendeleo kwa ajili ya
mchezo huo huku wakiendelea na mashindano.
No comments:
Post a Comment