KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Mart Nooij ameteua kikosi cha wachezaji 26 wa timu ya taifa ya maboresho kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda itakayopigwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Januari 22, mwaka huu.
Akizungumza
jana wakati anataka kikosi hicho Nooij alisema kati ya wachezaji hao 10 ambao
wanatoka katika mikoa ya kanda ya ziwa wataweka kambi Mwanza na wengine 10
wanaotoka upande wa Dar es Salaam wataweka kambi hapo Dar es Salaam.
Alisema
kambi kwa ajili ya michuano hiyo itaanza rasmi Januari 18, mwaka huu ambapo
siku inayofuata watakwenda Mwanza kuungana na wengine kwa ajili ya kambi ya
pamoja.
“Mechi hiyo
ni muhimu kwetu kwani wachezaji ambao watafanya vizuri tutawapandisha kucheza
katika kikosi kikubwa,”alisema Nooij.
Wachezaji
walioteuliwa ni Aishi
Manula, Benedict Tinoko, Miraji Adam, Andrew Vicent, Michael Gadiel, Emmanuel
Semwanda, Joram Mgeveke, Edward Charles na Adam Salamba.
Wengine ni pamoja na Aboubakary Mohammed, Hassan Dilunga,
Hussein Malombe, Shiza Ramadhani, Omari Nyenje, Kelvin Friday, Alfred
Masumbakenda, Salim Mbonde, Atupele Green na Rashid Mandawa, Manyika Peter,
Salum Telela, Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Ndemla, Said Makapu na Simon
Msuva.
Aidha,
kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati
Tendaji ya Shirikisho la Soka Tanzani (TFF), Vedastus Lufano, kiingilio kwenye
mechi hiyo itakuwa sh. 20,000 kwa viti maalumu (VIP), viti vya kawaida sh.
10,000 na mzunguko ni sh. 3,000.
Lufano
aliwataja baadhi ya wachezaji wa Amavubi wanaotarajia kutua jijini Mwanza
Januari 21 kwa ndege ya Rwanda Air, kuwa ni Marcel Nzarora, Olivier Kwizera,
Sotel Kayomba, Ismail Nshutiyamagala , Emery Basiyenge na Michel Rushengoga.
Wengine ni Fitina Ombolenga, Janvier Mutijima, Haruna Niyonzima, Tean Baptista, Mugiraneza Savio, Nshuti Dominique, Patrick Sibomano, Jean Claude, Zagabe Andrew, Buteara Ernest , Sugira Danny, Ushengimana Betramed Iladukunda na Blenvue Mugenzi.
Lufano aliongeza kuwa taarifa iliyotumwa TFF kutoka Rwanda, Amavubi itaongozana na viongozi waliotajwa kuwa ni Stephen Costan, Vincent Mashami, Ibrahim Mugisha, Moussa Hakizimana, Nuhu Assouman, Boume Mugabe, Piere Baziki na Mkuu wa Msafara Bandora Felician.
Awali,
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura
alisema mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo
kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).
Mechi za
mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda
zinaanza Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment