Bao 2 za Olivier Giroud na 2 za Santi Cazorla zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 4-1 walipocheza kwao Emirates na Newcastle na kuwapandisha hadi Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 West Ham na Timu ya 3 Manchester United.
Ushindi huu ulileta ahueni kwa Mashabiki wa Arsenal ambao baadhi yao walimshangilia Meneja wao Arsene Wenger baada ya Wiki iliyopita kufungwa na kumtaka Wenger ang’oke.
Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Giroud kwa Kichwa baada ya Krosi ya Alexis Sanchez na kisha Cazorla kuwapa Bao la Pili katika Dakika ya 54 na Giroud kuipa Arsenal Bao la 3 Dakika ya 58 lakini Ayoze Perez alileta matumaini kwa Newcastle alipofunga Bao katika Dakika ya 63.Giroud aliporuka juu na kuifungia bao la kwanza Arsenal kipindi cha kwanza dakika 15.
Mpaka Mapumziko Arsenal 1-0 Newcastle United. Ni baada ya kupokea krosi kutoka kwa Alexis Sanchez.Hata hivyo Cazorla aliwakata maini kwa kufunga Penati ya Dakika ya 88 na kuipa Arsenal ushindi wa Bao 4-1.VIKOSI:
Arsenal wanaoanza XI: Szczesny, Bellerin, Debuchy, Mertesacker, Gibbs, Flamini, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Alexis, Welbeck, Giroud
Akiba: Martinez, Ajayi, Coquelin, Maitland-Niles, Campbell, Podolski, Sanogo
Newcastle wanaoanza XI: Alnwick, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Tiote, Colback, Gouffran, Perez, Ameobi, Cisse
Akiba: Anita, Haidara, Cabella, Vuckic, Riviere, Armstrong, Woodman
No comments:
Post a Comment