Kikosi cha Kinondoni |
Kikosi cha Arusha |
TIMU
ya soka ya mkoa wa Kinondoni, imeanza vema mashindano ya Copa-Coca-Colakwa
U-15, ngazi ya taifa baada ya kuifunga
Arusha mabao 3-1 kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam jana.
Arusha
ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 38 lililofungwa na mshambuliaji
Robert Philipo lakini mshambuliaji wa Kinondoni Rashid Kilongola alisawazisha
bao hilo katika dakika ya 48.
Baada
ya mabao hayo timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini bahati ilikuwa ya
Kinondoni kwani walifanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 85
lililofungwa na Rashid Kilongola.
Akizungumza
baada ya mchezo kocha wa timu ya Arusha, Mohamed Laiser alisifu kiwango cha
wachezaji wake na kusema wamefungwa kwa bahati mbaya kwani walitawala mchezo
kwa kipindi chote.
“Mchezo
uliokuwa mzuri na wachezaji wamecheza vizuri lakini tuna nafasi ya kusonga
mbele kwani timu yangu ni nzuri ila ni matokeo tu ya mpira hayo”, alisema
Laizer
Michuano
hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Fenella
Mukangara juzi, ambaye aliwashauri makocha wa timu kutumia michuano ya
Copa-Coca-Cola kama changamoto ya kuibua vipaji vipya katika timu zao kwa
wasichana na wavulana.
Copa-Coca-Cola
ni michuano pekee ambayo huanzia ngazi ya chini kabisa na baadaye ngazi ya
Taifa ikishirikisha mikoa yote ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar ambapo mwaka
huu katika kuonesha umakini kwenye umri wamewaondoa wachezaji 87 kutoka katika
mikoa ya Mbeya na Lindi kutokana na kudanganya umri.
Michuano
hii itafikia tamati mnamo Desemba 20, mwaka huu, katika Uwanja wa kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment