Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 13, 2014

NANI MTANI JEMBE: LEO NI LEO, YANGA NA SIMBA NANI KUIBUKA KIDEDEA TAIFA LEO?

LEO UWANJA wa Taifa Jijini Dar es Salaam Mashabiki wa Klabu Mahasimu zinazotoka Maeneo ya Kariakoo Jjini humo, Yanga na Simba, watafurika Uwanja kuona Timu zao zikivaana kwenye Dabi ya Kariakoo kugombea Nani Mtani Jembe 2 promosheni mahsusi ya Kilimanjaro Premium Lager. 

Kila Timu, kwa mujibu wa Udhamini huo, wanawajibika kushusha Vikosi vyao kamili vya Timu zao za Kwanza.
Timu zote hizi zimekuwa na Mazoezi makali wakiwa Kambini kwa Yanga kuwa chini ya Kocha wao toka Brazil, Marcio Maximo, wakiwa Jijini Dar es Salaam, na Simba kuwa kule Zanzibar chini ya Kocha kutoka Zambia, Ptrick Phiri. 

Kila Timu imeimarisha Vikosi vyao kwa hivi karibuni kuchukua Wachezaji wapya kwa Yanga kuwasaini Mchezaji kutoka Brazil Emerson Roque, Straika wa zamani wa Simba Danny Mrwanda aliekuwa akicheza Nchini Vietnam pamoja na Straika wa Liberia aliekuwa akicheza Nchini Cyprus, Kpah Sean Sherman.
Nao Simba wanae Mchezaji mpya kutoka Uganda ambae ni Straika hatari, Danny Sserunkuma. 

Akifafanua kuhusu Mechi hii, Mkurugenzi wa Mashindano, Boniface Wambura, alisema Klabu zote zitaruhusiwa kuwatumia Wachezaji wao wapya waliowasajili kwenye Dirisha hili la Usajili na pia kwenye Mechi kila Timu kuruhusiwa kubadili Wachezaji Watano badala ya Watatu. 
Mgeni rasmi kwenye Mechi ya Pili ya Promosheni ya Nani Mtani Jembe anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Dr. Fenella Mikangara.
Mwaka Jana Simba iliifunga Yanga 3-1 kwenye Promoshini hii.

No comments:

Post a Comment