Real Madrid Jana wamepata ushindi wao wa 20 mfululizo katika Mashindano yote huku Cristiano Ronaldo akipiga Bao 2 wakati walipoifunga Ugenini Almeria Bao 4-1 katika Mechi ya La Liga.

Hadi Mapumziko, Real walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Isco na Gareth Bale Kwenye Mechi hiyo, Kipa Iker Casillas aliokoa Penati iliyopigwa na Verza.


Juzi Jumanne, Real walivunja Rekodi ya Barcelona ya kushinda Mechi 18 mfululizo walipoifunga Lugorets kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.

wamebeba Makombe ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Copa del Rey. Hivi sasa Real wapo Pointi 5 mbele ya Barcelona kwenye La Liga.

RATIBA/MATOKEO
Ijumaa Desemba 12
UD Almeria 1 Real Madrid CF 4
Jumamosi Desemba 13
18:00 Getafe CF v FC Barcelona
20:00 Valencia C.F v Rayo Vallecano
22:00 Cordoba CF v Levante
Jumapili Desemba 14
0:00 Malaga CF v Celta de Vigo
14:00 RCD Espanyol v Granada CF
19:00 Sevilla FC v SD Eibar
21:00 Atletico de Madrid v Villarreal CF
23:00 Real Sociedad v Athletic de Bilbao
Jumatatu Desemba 15
22:45 Deportivo La Coruna v Elche CF
Ijumaa Desemba 19
22:45 Celta de Vigo v UD Almeria
No comments:
Post a Comment