Mtoto wa Miaka 8, Martha Godfrey amejinyakulia kitita cha Tsh Milioni Moja leo baada ya kuwabwaga wenzake watano walioingia tano bora katika Shindano la kusoma Biblia hapa Mkoani Kagera. Shindano lililokuwa likishindaniwa na watoto walio Chini ya Umri wa Miaka 15 ambalo lilishirikisha Wilaya mbalimbali za hapa Mkoani Kagera. Wilaya zilizoshiriki ni Muleba, karagwe na Misenyi na katika mashindano hayo kumalizikia hapa Bukoba Mjini kwa Kumpata Mshindi kwenye Fainali iliyokuwa ya kukata na shoka iliyofanyika leo katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Watoto walioingia fainali na hatimae kumpata mshindi ni Neema Masembejo, Jonathan Kasika, Enock Joel, Neema Jackson na Martha Godfrey. Fainali hizo zilipambwa na Wasanii mahili wa Nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es salaam. Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula. Ambao walilipamba vilivyo Shindano hilo na kuhudhuriwa na Umati wa Watu wengi wakiwemo Viongozi wa Dini na wa Siasa. Katika Shindano hilo watoto wengi walishiriki lakini waliweza kupatikana Watoto 5 ambao waliingia hatua ya Fainali na kupata washindi watatu na hatimae kumpata mshindi Martha Godfrey. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mashindano haya ya Kusoma Biblia ni ya Kwanza kwa Mkoa wa Kagera na yaliandaliwa na Radio Kasibante fm 88.5 kupitia kipindi chake cha Gospal Flava na Mdhamini Mkuu ambaye pia ndie alikuwa Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini maarufu 'swahiba' Mh. Balozi Khamis Kagasheki. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini maarufu 'swahiba' Mh. Balozi Khamis Kagasheki akitoa neno mbele ya Umati Mkubwa wa Watu waliojitokeza kwa Wingi wakati wa Fainali za Shindano la Biblia kwa Mkoa wa Kagera leo Jumapili.
Gaston sapula akiwaburudisha kwa nyimbo za dini Mashabiki!Gaston Sapula na Vijana wake wakitoa Burudani Wimbo wake wa Mbuyu ulianza kama mchicha ukishika kasi! Vijana na Bosi wao wakiendesha!!
Kauli mbiu yao ikiwa inatoka Mithali 10:1 -Mwana mwenye hekima humfurahisha Babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye.Mtoto Martha Godfrey ambaye alishinda Sh Milioni moja kwenye Fainali ya kusoma Biblia ambapo yeye alitoa somo lake kutoka Kumbukumbu la Torati 4:1-10Jonathan KasikaNeema JacksonNeema Masembejo, Jonathan kasika, Martha Godfrey, Enock Joel na Neema Jackson wote walitinga hatua ya fainali hiyo na Martha mwenye umri wa miaka 8 akaibuka kidedea katika shindano hilo la kusoma biblia huku kila mmoja akisoma somo ambalo lilikuwa halifanani na mwingine mstari wa kwanza mpaka wa kumi. Picha na Faustine Ruta, Bukoba. Watoto hao walifanya vyema sana katika Usomaji wa Biblia na ikiwa ni mara yao ya kwanza katika shindano hilo.
Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege (Bony) akiimba nyimbo kwa hisia mbele ya mashabiki wake kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini kwenye Fanali za Biblia leo Jumapili.
Henry Mwaibambe(RPC) alimtuza Ndugu yake Bony MwaitegeMbunge wa Bukoba Mjini "Swahiba" Mh. Khamis kagasheki akimtuza Bony Mwaitege Uwanjani kaitaba baada ya kuburudishwa na mwimbaji huyo nyota wa Nyimbo za kumsifu Mungu.
Henry Mwaibambe(RPC) alimtuza Ndugu yake Bony MwaitegeMbunge wa Bukoba Mjini "Swahiba" Mh. Khamis kagasheki akimtuza Bony Mwaitege Uwanjani kaitaba baada ya kuburudishwa na mwimbaji huyo nyota wa Nyimbo za kumsifu Mungu.
Hatarii tupu!Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akifanya yake na Madancer wake
Mratibu Joys Roboz hakupimika alipokuwa!!
Mashabiki waliingia kwa Wingi
Kwa Makini wakisikiliza na kuburudika kwa nyimbo za injili.
Mashabiki wakimtuza Bony Mwaitege.
Furaha kwa Mashabiki'
Kwa Umahiri mkubwa wa Msanii wa Nyimbo za Injili Bony Mwaitege aliweza kujizolea sifa kutoka kwa Mashabiki wake baada ya kuimba Wimbo wake Mpya.
Shabiki alitoa zawadi ya Senene kwa Bony Mwaitege na ndipo mwimbji Gaston Sapula na Bony kuzichangamkia hapo hapo "Live bila chenga"
Mashabiki Jukwaa kuu wakiangalia zoezi la kula Senene likiendelea kushika kasi wakati wa Fainali za Biblia.
Kwa swala zima la Dini hata babu alitinga uwanjani kushuhudia Vijana wakiwajibika kutoa Neno Mambo ya Bukoba hayaKaribu!! Gaston Sapula(kushoto) na Bony wakishikamana kwa zoezi zima la kuchangamkia zawadi waliyopewa ya Senene!
Mbunge wa Bukoba Mjini Balozi Khamis kagasheki(kulia) akiwa meza kuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Viongoz mbalimbali wa Dini walijitokeza katika fainali za Kusoma Biblia zilizofanyika kwa mara ya kwanza hapa Bukoba.
Mratibu wa Shindano hilo Joyce Roboz akifurahia baada ya kukunwa na nyimbo mbalimbali kutoka kwa wasanii hao wakali kutoka jijini dar es Salaam. shindano hilo liliandaliwa na ikiwa ni Ubunifu wake mwenyewe Joyce Roboz na kufankiwa kuchukua sura mpya hapa Bukoba na kuwafanya baadhi ya Wananchi kutoamini jambo hilo kama linaweza kufanyika.
Diwani Mulungi nae furaha tupu!
Zungusha!!! Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akitimua vumbi!!
Brother Samwel na Mkewe walipokuwa ni furaha tupu...wakiburudishwa na Mwaitege
Muimbaji wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akicheza na Vijana wake.
Bony Mwaitege alimtuza mwimbaji mwenzake wa injili ose Muhando.
Rose Muhando nae aliingia kwa salamu salamu za Kiface book!!Rose Muhando akiendelea kutoa burudani kwa Wakaazi wa Bukoba waliohudhuria Shindano hilo kwenye Uwanja wa kaitaba.Nani zaidi???Watatu ndani ya kaitaba!!Rose Muhando akicheza na Shabiki wake Rose Muhando na Vijana wake wakitawala sehemu yao!
Washindi wakiwa wameonesha Vitita Vyao(pesa) walizojishindia leo kwenye Fainali za Mashindano hayo. Na hapa ni kwenye picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mh. Balozi Khamis Kagasheki.
No comments:
Post a Comment