Louis
van Gaal amesimikwa kama ndie Kocha Bora wa Mwaka huko kwao Holland
baada ya kuiongoza vyema Nchi yake kufika Nusu Fainali za Kombe la Dunia
huko Brazil Mwezi Julai. Van
Gaal, ambae aling’atuka kama Kocha wa Holland mara baada ya Kombe la
Dunia na kutua Manchester United kama Meneja mpya, alipewa Tuzo yake
hiyo ya juu hapo Jana huko Mjini Amsterdam wakati wa Hafla maalum ya
Wanamichezo. Van
Gaal ndie aliekuwa kiini cha kuiongoza Holland kufika Nusu Fainali za
Kombe la Dunia huko Brazil ambapo walitolewa kwa Mikwaju ya Penati na
Argentina lakini wakafanikiwa kutwaa Nafasi ya 3 kwenye Kombe la Dunia
baada ya kuichapa Brazil 3-0. Kocha
huyo mwenye Miaka 63 ambae pia aliwahi kuiongoza Holland kati ya Mwaka
2000 na 2002 alihamia Man United Mwezi Julai na kumwachia wadhifa wa
kuiongoza Holland Guus Hiddink. Sambamba
na Van Gaal kutwaa Tuzo, Mchezaji wake wa Man United na ambae pia ni
Nahodha wa Holland, Robin van Persie, nae pia alitunukiwa Tuzo kwenye
Hafla ya hiyo Jana. Van
Persie alipewa Tuzo ya Mchezo Bora wa Mwaka kutokana na Bao lake safi
alilofunga kwa Kichwa wakati Holland inawatwanga waliokuwa Mabingwa wa
Dunia Spain Bao 5-1 katika Mechi ya ufunguzi ya Kundi lao kwenye Kombe
la Dunia huko Brazil Mwezi Juni.
Bao hilo pia lipo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya FIFA ya kuwania Bao Bora la Mwaka Duniani ambapo Mshindi wake kati ya Wagombea Watatu atatangazwa Januari 12.
Bao hilo pia lipo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya FIFA ya kuwania Bao Bora la Mwaka Duniani ambapo Mshindi wake kati ya Wagombea Watatu atatangazwa Januari 12.
No comments:
Post a Comment