Mastaa
waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole wakiongea na wanahabari
(hawapo pichani) jinsi walivyopania kufanya kweli kwenye uzinduzi wa
kundi lao jipya la Kaone, Boxing Day ndani ya Dar Live.
Muhogo Mchungu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni msanii Thea.
Wasanii hao wakongwe wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo na wanahabari. Mkutano huo umefanyika leo katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Dar.
Msanii Thea (kulia) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Msanii Kingwendu akitoa burudani wakati akiongea na mwanahabari wa TBC.
ZIKIWA
zimesalia siku chache kuelekea ule Usiku wa Wasanii Wakongwe Desemba 26
‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo
Mbagala-Zakhem, jijini Dar, mastaa kibao waliokuwa wakiunda kundi la
zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya linalojulikana kama Kaone.
Usiku
huo utakaokuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka
Kaole kama vile Swebe, Davina, Koletha, Zawadi, Nyamayao, Kingwendu,
Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine kibao ambao kwa mara ya kwanza
watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa
itakayoanza kuruka hewani Januari 4, 2015 ndani ya Runinga ya TV1.
Usiku
huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha pamoja na
Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.
Mapema
kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi
la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo,
mazingaombwe sambamba na kutoa zawadi kibao huku watoto wengine wakipata
nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.
No comments:
Post a Comment