Taasisi
inayopambana na ubaguzi wa rangi wa 'Kick It Out' imelitahadharisha
jeshi la polisi juu ya ujumbe wa kibaguzi wa rangi kupitia akaunti ya
twitter ya kiungo wa Manchester City Yaya Toure baada ya mchezo wa
Jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jiji la Manchester Manchester United.
Kiungo
huyo alilazimika kuufunga kwa muda ukurasa wake huo kabla ya kurudishia
uhai Jumatatu ikiwa ni siku moja baada ya mchezo wa ushindi wa 1-0
dhidi ya Manchester United.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast aliandika katika ukurasa wake huo
"Great to be back on Twitter after a good win
yesterday. Now my focus is on the next game...Happy Monday everyone!!"
Katika
taarifa yake Jumanne ya leo, Kick It Out imesema kuwa Toure alipokea
ujumbe wa kumbagua muda mfupi baada ya kutupia ujumbe ambapo ulionekana
kuwakwaza baadhi ya wanaomfuata.
Msemaji
wa Kick It Out amesema "tumepokea malalamiko kutoka katika jumbe mbili
za tweeter zikimdhihaki kwa rangi Yaya Toure usiku wa jana.
"tumewaarifu polisi kupitia 'True Vision', kwa njia ya mtandao na tayari wamewatahadharisha Twitter.
No comments:
Post a Comment