Shirikisho
la soka duniani (FIFA) imetaka mchezo uliopangwa baina ya Uganda na
Sudan kuondolewa katika mpango wa kuchezwa. Katende Malibu, afisa habari
wa Uganda Cranes
amesema.
"Hatutacheza mchezo wa kirafiki na Sudan kwa amri ya FIFA, hivyo mchezo wetu dhidi ya Ethiopian uko kama ulivyopangwa"
Shirikisho
la soka la Uganda(FUFA) lilipanga mchezo dhidi ya Sudan uchezwe Jumanne
Novemba 11 2014 ikiwa ni siku mbili baada ya mchezo wao dhidi ya
Ethiopia tarehe 9 Novemba 2014
Mchezo wa Ethiopia uliandaliwa na Serikali ya nchi hiyo kupitia wizara mbili za Elimu na Wizara ya michezo na Afya.
Taarifa kutoka Zurich zimesema kuwa michezo miwili ya kujipima nguvu ilikuwa imepangwa kuchezwa kinyume na sheria za FIFA na kwamba hilo halitaruhusiwa ndani ya siku mbili.
Kuelekea
mchezo dhidi ya Ethiopia kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin
‘Micho’ Sredojevic tayari ameshakamilisha orodha ya wachezaji
watakaocheza mchezo huo na wengi wakitokea katika ligi ya nchi hiyo
"Uganda Premier League".
Wachezaji watano wanaochezea katika ligi za Kenya na Ethiopia pia wamejumuishwa kikosini ambapo Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta
Museveni atakuwa mgeni wa heshima na hakutakuwa na kiingilio.
No comments:
Post a Comment