Straika
wa Liverpool Daniel Sturridge ameanza tena Mazoezi tangu aumie Musuli
za Pajani [Hamstring] Mwezi Agosti akiwa na Timu ya Taifa ya England.
Kukosekana kwa Straika huyo ambae ndie amegeuka mtambo wa Magoli wa Liverpool kumewafanya washinde Mechi 4 tu kati ya 14 ambazo amezikosa.
Sturridge, ambae alifunga Bao 21 katika Mechi 29 za Ligi Msimu uliopita, alikaribia kurejea Uwanjani Mwezi uliopita lakini akapata maumivu mengine Mguuni yaliyomweka nje kwa kipindi kingine.
Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers anategemea Sturridge atakuwa fiti kucheza Mechi yao inayokuja ya Ugenini ya Ligi Kuu England na Crystal Palace hapo Novemba 23.
Msimu huu, Sturridge amecheza Mechi 3 tu za Ligi na kufunga Bao walipocheza Anfield Agosti 17 na kuifunga Southampton 2-1.
Kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, Liverpool wapo Nafasi ya 11 wakiwa Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea na hawajashinda katika Mechi 3 zilizopita.

No comments:
Post a Comment