Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya ukufunzi wa waamuzi ya FUTURO III ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Hafla ya ufunguzi
wa kozi hiyo inayoshirikisha zaidi ya waamuzi 40 wakiwemo baadhi ya wale ambao
bado wanachezesha mpira wa miguu kutoka nchi mbalimbali za Afrika itafanyika
saa 4 asubuhi kwenye hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.
Kati ya hao,
washiriki wanane wa kozi hiyo inayoanza kesho hadi Novemba 3 mwaka huu chini ya
wakufunzi wa FIFA wakiongozwa na Carlos Henriques ni kutoka Tanzania.
Washiriki kutoka
Tanzania ni Emmanuel Chaula, Joan Minja, Josephat Bulali, Paschal Chiganga,
Ramadhan Ibada, Richard Kayenze, Samuel Mpenzu na Soud Abdi.
No comments:
Post a Comment