

Jumatano yapo mapambano mawili ya Timu za Ligi Kuu England pekee ambayo ni huko Etihad kati ya Mabingwa wa England na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Man City, dhidi ya Newcastle, na jingine ni lile la Stoke City v Southampton.

Siku hiyo hiyo, Tottenham watakuwa kwao White Hart Lane kucheza na Brighton City ambayo inacheza Daraja la Championship ambalo ni chini tu ya Ligi Kuu England.

Washindi wa Raundi hii ya Nne watatinga Robo Fainali ambayo Droo yake itafanyika kesho kutwa na Mechi zake kuchezwa Wiki ya Desemba 14.

CAPITAL ONE CUP
RAUNDI YA 4
RATIBA
Jumanne Oktoba 28
22:45 Bournemouth v West Brom
22:45 MK Dons v Sheffield United
22:45 Shrewsbury v Chelsea
2300 Fulham v Derby
2300 Liverpool v Swansea
Jumatano Oktoba 29
22:45 Man City v Newcastle
22:45 Stoke v Southampton
22:45 Tottenham v Brighton
FAINALI
Jumapili 1 Machi 2015
No comments:
Post a Comment