Kiungo wa timu
ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali
nchini.
Abubakar ambaye
pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji
wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji hao ni
Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera
Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa kuibuka
mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh. milioni moja
kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la
makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi
kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili
kumpata mshindi wa mwezi.
No comments:
Post a Comment