Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 19, 2014

YAYA TOURE AWACHEFUA MASHABIKI KWA KUMKUMBATIA PEP GUARDIOLA

MASHABIKI wa Manchester City wamemjia juu Mchezaji wao Yaya Toure kwa kitendo chake cha kukumbatiana kwa furaha na Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola Jumatano Usiku Uwanjani Allianz Arena mara tu baada ya City kuchapwa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.Huku Wachezaji wenzake wa City wakikumbwa na majonzi makubwa baada ya kufungwa Bao la Dakika ya 89 la Shuti kali la Jerome Boateng, Toure alitoka Uwanjani na kwenda moja kwa moja kucheka na kukumbatiana na Guardiola ambae alikuwa Kocha wa Barcelona wakati Toure anachezea Timu hiyo huko Spain.
Kitendo hicho kiliamsha hisia kali za Mashabiki wengi wa Man City ambao walivamia Mitandao ya Kijamii na kumshutumu vikali Kiungo huyo ambae pia amedaiwa kucheza chini ya kiwango kwenye Mechi hiyo.
Hadi sasa Man City imekataa kuzungumza chochote kuhusu sakata hili lakini inategemewa Toure atacheza Mechi yao ijayo Uwanjani Etihad watakapoivaa Chelsea kwenye Mechi ya Ligi Kuu England hapo Jumapili.Yaya Toure akiwa hoi baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Bayern Munich
BAYERN vs CITY DISTANCE STATS 
Alonso 12.09km (7.51 miles)
Alaba 11.44 (7.11)
Gotze 11.41 (7.09)
Lahm 11.29 (7.02)
Silva 11.10 (7.02)
Navas 11.07 (6.88)
Toure 10.89 (6.77)
Fernandinho 10.65 (6.62)
Sagna 10.37 (6.44)

No comments:

Post a Comment