Washiriki wa shindano wakiwa kwenye picha ya pamoja |
Mshindi wa pili akiwa na zawadi zake |
Shindano hili ambalo lilivuta umati mkubwa wa watu japo
kulikuwepo mvua za hapa na pale lilifanyika katika viwanja vya Tanganyika Parkers,
Kawe jijini Dar es Salaam leo.
Nafasi ya pli ilichukuliwa na Ramadhani Ahmad Danga na
nafasi ya tatu ilikwenda kwa Winston Rwegalulila Rwechungura ambao wote kwa
pamoja walipata nafasi ya kwenda nchini
Afrika Kusini kushiriki faibnali
za Scania ambazo zitahusisha madereva wan chi zilizo kusini mwa jangwa la
Sahara.
Akizungumza wakati akikabidhi zawadi kwa washindi, Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna
Msaidizi wa
Polisi, Johansen Kahatano aliwapongeza madereva alishinda na kuwataka kuwa
mfano bora kwa utii wa sheria barabarani.
“Nawapongeza madereva wote kwa kushiriki shindano hili
lakini kipekee kwa washindi watatu wa mwanzoni na naowaomba muwe mabalozi
wazuri wa utii wa sheria barabarani si kwamba muishie hapa kwenye shindano”,
alisema Kahatano.
Pia aliipongeza kampuni ya Scania kwa kuendesha
shindano hili kwani litaibua hari kwa
madereva wengine kushiriki na kuwa chachu wa utii wa sheria za barabarani jambo
ambalo litaepusha ajali za barabarani ambazo zinazepukika.
Naye Afisa mwendeshaji wa Scania Kisali Nnyari, alisema kuwa
washndi watatu wa juu watagharamia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini wao na
wenzao wao pamoja na bosi wa kampuni yake kwa siku saba kuanzia malazi, chakula
na usafari wa kwenda na kurudi.
Sehemu ya umati uliofika kushuhudia |
Shindano hili linafanyika kwa mara ya pili hapa nchini na
limeacha gumzo kwa watu waliojitokeza kushuhudia huku madereva wengine wakiomba
kuingizwa kwenye orodha ya washiriki bila kupitia hatua za awali jambo ambalo
lilishindikana kukutokna na sheria za shindano lenyewe.
No comments:
Post a Comment