Inavyoonekana ni kuwa mashabiki wa soka huwa hawapati nafasi ya angalau kukutana na mashujaa wao wanaowapenda, hii ni tofauti kwa klabu ya Villarreal ambayo yenyewe imetoa nafasi kwa mmoja wa shabiki wake kutimiza ndoto yake ya kuichezea klabu hiyo.
Klabu
hiyo kubwa nchini Hispania ilikuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
Celtic hivi karibuni na kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza dogo
mwenye umri wa miaka 13 ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kansa Gohan.
Hapo
kabla Gohan aliwafahamisha manesi wanamuhudumia kuwa ana ndoto ya
kuichezea Villarreal ndani ya uwanja wa Madrigal huku nayo klabu hiyo
ikalipokea hilo kwa furaha.
Villarreal
imekubali kulipia gharama zote za matibabu ya daraja la VIP kwa Gohan
alipokutana na wachezaji katika chumba cha kubadilishia nguo kabla ya
mchezo wa Hisani kuchangia watoto wanao sumbuliwa na kansa ambapo
wachezaji walifurahishwa mno kukutana naye na kuwa nyuma yake.
Usiku
huo ulikuwa mzuri kwa dogo huyo ambaye alifunga goli kupitia mpira wa
adhabu ya moja kwa moja baada ya kuonyesha utundu wa kuchezea mpira.
Akifurahia
goli hilo alilofunga na wachezaji wenzake wa Villarreal baadaye Gohan
alibadilishwa huku akipokea makofi mengi ya mashabiki wa klabu hiyo
ambayo ilishinda bao 5-2.
Gohan alifunga goli la kwanza la Villarreal na kupongezwa na wachezaji wenzake
Wachezaji wa Villarreal wakimbeba Gohan baada ya kufunga goli la kwanza
Tabasamu: Gohan anakutana na mashujaa wake wa Villarreal kabla ya mchezo kuanza
Timu
hizo mbili zilikubaliana kuunganisha nguvu katika miaka ya hivi
karibuni kwa lengo kutunisha mfuko wa kuhudumia watoto wenye kusumbuliwa
na maradhi ya kansa.
Kichocheo
kikubwa cha makubaliano hayo kilikuwa ni Mchezaji wa zamani wa
Villarreal Ernesto Boixader alipoteza mtoto wake kutokana na maradhi
hayo kabla ya mchezo wa UEFA Cup dhidi ya Celtic miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment