Hatua ya makundi ya kufuzu kwa fainali za kombe la
mataifa ya Afrika inaanza ijumaa hii ambapo mataifa 28 yanawania nafasi
15 za kuungana na wenyeji Morocco ili kushiriki michuano hiyo.
Maandalizi yamekumbwa na msukosuko kutokana na
mlipuko wa Ebola kiasi cha Shirikisho la soka Afrika kuziamuru Guinea na
Sierra Leone kubadili viwanja vyao vya nyumbani na kulazimika kucheza
kwingine.
Wenyeji wamesumbuliwa na majeraha kadhaa akiwemo Florentin Pogba kaka wa mchezaji wa Ufaransa Paul Pogba.
Pia wanakosekana kiungo wa Lorient Abdoulaye Sadio Diallo na mshambuliaji wa Lyon Mohamed Lamine Yattara.
Togo imeongezewa nguvu kutokana na kurejea kwa mshambuliaji wao Emmanuel Adebayor ambaye amekuwa nje kwa miezi 18.
Mshambuliaji huyo wa Tottenham Hotspur mwenye
miaka 30 mwaka jana alikataa wito wa kushiriki kufuzu kombe la dunia
kutokana na kutokuelewana na kocha Didier Six baada ya michuano ya kombe
la afrika mwaka 2013.
Hata hivyo alipata majeraha kidogo wakati wa
mazoezi ya Togo huko Lome jumatano hii hali iliyoleta hofu kuwa anaweza
kukosa mchezo wao huko Casablanka
Timu nyingine mbili Ghana na Uganda wanakutana Kumasi jumamosi.
Mchuano mkali wa kwanza wa aina yake kwa kundi A ni kati ya Sudan na Afrika ya Kusini.
Kocha mpya wa Bafana Bafana Ephraim 'Shakes'
Mashaba atalazimika kuingia uwanjanai bila mlinda mlango wake Itumeleng
Khune ambaye amepata ajali ya mguu.
Ambaye pia anaikosa safari kuelekea Khartoum ni
kiungo wa Lokeren Ayanda Patosi ambaye alishindwa kufika baada ya
kushindwa kuunganisha kutoka Belgium.
Mlinda mlango Itumeleng Khune ataikosa mechi ya Afrika Kusini dhidi ya Sudan
“Ninafurahia kuwa na kundi hili la wachezaji ninaosafiri nao. Tunaenda kupambana, hakuna kufanya makosa alisema Kocha Mashaba.
Ili kukwepa kuchelewa kwa usafiri, Afrika Kusini wameamua kukodi ndege itakayowapeleka Sudan na kuwarudisha nyumbani.
Sudan iliupoteza nchezo wake wa kirafiki dhidi
ya Zambia kwa kuchapwa bao 3-1 katika uwanja mpya wa mashujaa wenye
kuweza kubeba watu elfu 50 pale Lusaka.
Mabingwa wa Afrika Nigeria wanawaalika Congo Brazzaville jumamosi katika mchuano mwingine wa kundi A.
Super Eagles wanacheza wakiwa na hofu ya
kufungiwa kushiriki soka la dunia iwapo Chris Giwa hatalegeza msimamo
wake wa kuendelea kudai yeye ndiye rais wa shirikisho la soka la nchini.
Mechi ya mwisho ijumaa ni katika ya Senegal dhidi ya washindi wa kombe la afrika mara 7,Misri.
Zote mbili hazikufuzu katika michuano ya mwaka
2013 huko Afrika ya kusini na misri ilikosa michuano huko Equatorial
Guinea na Gabon.
Kocha Shawky Gharib msaidizi wa Hassan Shehata
ameweka mkazo zaidi katika vijana lakini amempa nafasi Mlinda mlango
mkongwe mwenye miaka 41 Essam Al Hadary.
Ni mechi ya kwanza kamili ya kimataifa huko
Senegal tangu mwaka 2012 baada ya vurugu zilizovunja mechi yao dhidi ya
Ivory Coast wakati wa kuelekea katika kombe la dunia.
Hali hiyo ilifuatiwa na kufungiwa kwa mwaka
mmoja uwanja wa Leopold Sedar Senghorna. Tangu kumalizika kwa adhabu
hiyo ni michuano ya ndani ya afrika iliyofanyika Dakar
Tunisia wanawakaribisha Botswana jumamosi katika
kundi G. Timu mbili za kwanza katika kila kundi kutoka katika makundi
yote 7 na timu moja ya tatu kwa ubora zitajiunga wenyeji Morocco
kukamilisha timu 16 tayari kwa michuano mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment