Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mheshimiwa Said Mtanda anatarajia
kufunga kozi ya ukocha ya Leseni A ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
inayomalizika kesho (Septemba 7 mwaka huu).
Hafla
hiyo ya ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 22 itafanyika saa 7
mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.
Kozi
hiyo ya siku tano iliyokuwa chini ya wakunzi wa CAF, Moatasim Mohamed Nasr
kutoka Sudan na Sunday Kayuni wa Tanzania.
KOZI YA
UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA KUFANYIKA DESEMBA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika
Desemba mwaka huu.
Kozi
hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka
kushiriki ni kidato cha nne.
Kwa
wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa
TFF. Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 12 mwaka huu ambapo wanatakiwa
pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma.
No comments:
Post a Comment