Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 25, 2014

MASHABIKI WAPANIA KUMRUDISHA RONALDO MAN UNITED, KURUSHA NDEGE BERNABEU YENYE BANGO ‘RUDI NYUMBANI RONALDO’

HUKU akihusishwa sana na kurejea Klabu yake ya zamani Manchester United, Mashabiki wa Klabu hiyo wamepanga kurusha Ndege juu ya anga ya Santiago Bernabeu wakati Real Madrid inacheza na Villareal hapo Jumamosi ikiwa na Bango kubwa: “RUDI NYUMBANI RONALDO – UNITED REEL”.United Reel, Kundi linalojitangaza kuwa wao ni ‘Mashabiki wa kufa na kupona wa Manchester United kutoka kila kona ya Dunia’, wamejichangisha Fedha kukodi Ndege hiyo ili ipeperushe Bango hilo la kumsihi Ronaldo arudi Old Trafford alikoondoka Mwaka 2009 kujiunga na Real Madrid.Supporters' group United Reel are planning a fly over plea duringthe game between Real Madrid and Villarreal

Tamko la Kundi hilo limesema: “United Reel lina Mashabiki walio hai kutoka kila Bara Duniani na tunaungana katika mapenzi yetu kwa Ronaldo kama Mchezaji na Mtu. Tuko pamoja na hatutapumzika mpaka tumrudishe Ronaldo Nyumbani.”
Hivi karibuni kulizuka habari kuwa Ronald ameonyesha nia ya kurudi tena Man United huku Rais wa zamani wa Real, Ramon Calderon, akidai Mchezaji huyo anataka aende Man United kwa sababu amechoshwa na Real kwa uamuzi wake wa kuwauza Mastaa wao ikiwa pamoja na Angel Di Maria ambae sasa yupo Man United.

Ijumaa iliyopita, akiongea na Wanahabari, Meneja wa Man United Louis Van Gaal alijibu swali kwamba upo uwezekano wa wao kumchukua Ronaldo.

Van Gaal alisema: “Ndio lakini haya ni mazungumzo ya Magazeti na sidhani kama Vyombo vya Habari vitamnunua!”

Alipokazaniwa kujibu swali hilo, Van Gaal alisema: “Inawezekana. Nilisema hivyo hivyo kwa Falcao. Wachezaji kama Ronaldo wanaleta mambo mengi kwenye Timu lakini sidhani kama Real watamuuza!”

Ronaldo, mwenye Miaka 29, alitwaa Mataji 8 akiwa chini ya Meneja Sir Alex Ferguson na Mwaka 2009 aliuzwa kwa Real kwa Dau la Rekodi ya Dunia kwa wakati huo la Pauni Milioni 80.

Mwezi uliopita, Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, alikiri angefurahia kurudi Man United pale aliposema: “Naipenda Manchester na huwezi kujua katika Soka. Ni kweli nina furaha hapa Real, ni nyumbani, ni Klabu yangu, lakini United walinitendea wema sana, na huwezi kujua!”

Aliongeza: “Bado nina mawasiliano na baadhi ya Watu huko kwa sababu nllikuwa na uhusiano mzuri na kila Mtu – ni kama Familia yangu ya pili!”

No comments:

Post a Comment