Guardiola anaamini kuwa kushindwa kwa Manchester United kutinga ligi ya mabingwa Ulaya ni somo kwa timu kubwa Ulaya |
Bosi
wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema kuanguka kwa kigogo cha soka
duniani klabu ya Manchester United kutoka katika zama za mafanikio ni
onyo kwa vilabu vingine vikubwa barani Ulaya na kutanabaisha kuwa klabu
hiyo yenye maskani yake Old Trafford haikuwa na nguvu ya kutosha
kuwasajili wachezaji wake katika kipindi cha usajili cha majira ya
kiangazi.
United
imeshindwa kutinga katika ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya jambo
ambalo limekuwa ni mshituko mkubwa kote barani humo na Guardiola
anaamini kuwa hakuna klabu yoyote kubwa itakayoweza mbele yao kama
ilivyokuwa kwa United.
“Sisi
ni timu isiyofungika na tuko imara bahati mbaya kwao hawapo katika ligi
ya mabingwa pengine msimu ujao" amesema bosi huyo wa zamani wa
Barcelona.
Van Persi wa Manchester United atakuwa mtazamaji wa ligi ya mabingwa Ulaya |
‘Hivi ndivyo ilivyo katika mchezo wa mpira wa miguu, ni mchezo wa ajabu.
‘Kila wiki unapaswa kuwa tayari, kila wiki unapaswa kuwa tayari.’
Guardiola pia amethibitisha kuwa Louis van Gaal alijaribu kuwasajili wachezaji wake Arjen
Robben, Bastian Schweinsteiger na Thomas Mueller kiangazi yote lakini United walishindwa kumudu hilo.
‘Hawakuwa na pesa ya kutosha kumsajili mchezaji huyo'.
No comments:
Post a Comment