Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 26, 2014

LIVERPOOL YACHUNGUZWA NA UEFA KWA KUKIUKA FFP

UEFA Leo imethibitisha kuwa Liverpool ni moja ya Timu 7 ambazo zinachunguzwa kwa kukiuka FFP [Financial Fair Play] ambayo hutaka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe.
Chini ya Sheria hizo za FFP za UEFA, Klabu ambazo zinashiriki Mashindano ya Ulaya zinatakiwa zidhibiti Hasara zisizidi Pauni Milioni 35.4 kwa Misimu miwili.
Mbali ya Liverpool, Klabu nyingine ambazo zinachunguzwa ni AS Monaco, Inter Milan, AS Roma, Besiktas, Sporting Lisbon na Krasnodar.
The Reds are hoping to write off proportion of losses as allowable stadium expenditure
Mwezi Mei, Manchester City na Paris St-Germain ziliadhibiwa na UEFA kwa kukiuka FFP kwa kupigwa Faini na pia Vikosi vyao vinavyocheza Ulaya kupunguzwa.
Klabu hizo 7 zimetakiwa na UEFA zipeleke Makabrasha ya ziada Mwezi Oktoba na Novemba kabla UEFA haijaamua Adhabu ipi zipewe.
Msimu wa 2012/13 Liverpool ilipata Hasara ya Pauni Milioni 49.8 na Msimu wa 2011/12 Hasara yao ilikuwa Pauni Milioni 41.

Msimu uliopita, Klabu 76 zilichunguzwa na UEFA lakini ni Klabu 9 tu ndizo ziliadhibiwa.

Kanuni za FFP zimeanza kutumika rasmi Msimu huu baada kuwa na Kipindi cha Mpito cha Miaka Mitatu na, kimsingi, zinataka Klabu zisitumie Fedha zaidi ya Mapato yao yanayotokana na Haki za TV, Tiketi Milangoni, Udhamini na Zawadi za Ushindi kwenye Mashindano.

Ingawa Mfumo huo unaruhusu Madeni kwa kiwango fulani lakini upo mahsusi kuzuia Matumizi mabovu ya Klabu kwenye Mishahara ya Wachezaji na Uhamisho wao wakitegemea Ruzuku toka kwa Wamiliki wao Matajiri.

No comments:

Post a Comment