Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi wa
daraja la kwanza (class one), Luteni David Lugenge kilichotokea jana (Septemba 7
mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Luteni
Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa mwili kwa
waamuzi wa Ligi Kuu alikuwa na ndugu yake Christopher Alexander Lunyungu katika
gari dogo wakienda mkoani Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Handeni, Peter Juma,
Luteni Lugenge alikuwa akimsindikiza mwenzake aliyekuwa anakwenda
kujitambulisha kwa wakwe zake watarajiwa.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Luteni Lugenge alikuwa ni
mmoja wa waamuzi wanaoinukia nchini, hivyo mchango wake ulikuwa bado unahitajika.
Hivyo tutamkumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira
wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
BONIFACE
WAMBURA
KNY KATIBU
MKUU
SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment