MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI wa Manchester United Ed Woodward amesema Klabu yao inakaribia kufanya kitu spesho.
Akiongea na Wawekezaji wa Klabu hiyo, Woodward alitangaza Mapato ya Klabu kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/14 kupanda kwa Asilimia 19 na kufikia Pauni Milioni 433.2.
Woodward alisema: “Msimu wa 2013/14 ulikuwa na changamoto sana na wa kusikitisha lakini sasa tunahamasika kumpata mmoja wa Mameneja bora Duniani na tunahisi kuna kitu spesho kitatokea!”
Licha ya kumaliza Msimu huo Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu England na kukosa Nafasi ya kucheza Ulaya, Man United imefanikiwa kuzalisha Mapato hayo makubwa na ya Rekodi na pia kuzidi kuvutia Wawekezaji Dunia nzima.
Mbali ya kutumia Pauni Milioni 150 hivi sasa kununua Wachezaji wapya wakiwemo Angel Di Maria na Radamel Falcao, Woodward alitoboa Meneja Louis van Gaal yuko huru kununua Wachezaji wengine Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.
Mmoja ambae upo uhakika wa kuchukuliwa Mwezi Januari ni Kiungo wa AS Roma na Holland, Kevin Strootman, ambae ni mmoja wa Walengwa wa Van Gaal.
Woodward pia alitoboa kuwa katika Mipango yao na Bajeti zao za baadae, Mizani zimechukulia kuwa Nafasi ya chini kabisa Man United watamaliza Msimu huu ni Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England.Marcos RojoAngel Di Maria
Daley Blind
No comments:
Post a Comment