NI
MSIMU MPYA wa Ligi Kuu England lakini kwa Washabiki wa Manchester
United umeanza kwa kuwakumbusha Msimu uliopita ambao walitaka kuusahau.
Baada ya kumpata Meneja mpya Louis van Gaal ambae katika Mechi 6 za Kirafiki kabla Msimu kuanza walishinda zote ukiwemo ushindi dhidi ya Vigogo AS Roma, Real Madrid na Liverpool, Jana Man United walikumubushwa tena ya Mwaka Jana chini ya David Moyes walipopigwa Bao 2-1 na Swansea City Uwanjani kwao Old Trafford katika Mechi ya kwanza kabisa ya Msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu England.
Kabla ya Mechi hiyo, Mashabiki wa Man United wenye matumaini makubwa waliingia Old Trafford wakiwa na Skafu na Tisheti zenye Ujumbe: “Mambo yatakuwa safi!” na “Mfalme Louis yuko hapa – United wamerudi!”
Lakini baada ya kipigo wote walinyong’onyea.
DONDOO:
-Mara ya mwisho Manchester United kuanza Msimu mpya na kufungwa Nyumbani kwao Old Trafford ni Msimu wa 1972/73 walipofungwa 3-2 na Ipswich Town!
Mashabiki hao walikumbushwa kwa uchungu kwamba David Moyes ameondoka lakini Timu iliyobaki ni ile ile kasoro kuondokewa Wachezaji zaidi wazoefu kina Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra.
Hiyo ni Timu Msimu uliopita ilimaliza Nafasi ya 7, Pointi 22 nyuma ya Mabingwa Manchester City.
Danny Mills, Mchambuzi wa BBC Radio 5:"Wako mbali na UEFA CHAMPIONS LIGI. Nimeshafanya Utabiri wangu kwamba watamaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi ikiwa watapata Wachezaji wapya. Timu haina Wachezaji wazuri. Ukiwaondoa Wayne Rooney, Robin van Persie na Juan Mata, nani yupo? Ed Woodward alipondwa sana Msimu uliopitwa kwa kutoleta Wachezaji wapya. Na safari hii tena watafanya kosa hilo hilo?"
Pengine Jana kuwa na Listi ndefu ya Majeruhi, kama vile Jonny Evans, Valencia, Welbeck na pia Mchezaji mpya Fulbeki Luke Shaw, na pia kumkosa Robin van Persie ambae ndio kwanza amerudi Mazoezini, kulichangia hasa baada ya Van Gaal kulazimika kuwatumia Chipukizi.
Miongoni mwa Chipukizi hao waliocheza Jana kwa mara ya kwanza kwenye Ligi ni Tyler Blackett na Jesse Lingard.
Lakini hilo, na utumiaji Mfumo mpya wa 3-4-1-2, ambao unahitaji Difensi ya Mtu 3 nzuri, ambayo Man United hawana, na Wachezaji wawili Mafulbeki-Winga, ambao Man United hawana wa kuridhisha, pengine ulichangia kipigo hicho.
NUKUU:
MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal:
"Inasikitisha tumefungwa Mechi yetu ya kwanza nyumbani. Hatukufikia kwenye kiwango tunachoweza kucheza. Hilo linasikitisha kwani tuna uwezo wa kucheza zaidi ya hapo lakini ukishindwa kufanya hivyo nyumbani inasikitisha hasa kwa Mashabiki wako. Tulikuwa na mchecheto hasa Kipindi cha Kwanza. Kipindi cha Pili hatukucheza kama Timu na kwa hilo nawajibika. Tulipata nafasi nyingi kupita Swansea lakini hilo halisemi lolote kuhusu matokeo. Ni Magoli ndio muhimu. Ilipokuwa 1-1 nilihisi tutashinda lakini kwa sababu hatukucheza Kitimu tulikuwa tukifanya makosa wakati tukienda mbele kushambulia. Wachezaji walijitahidi lakini wanatakiwa wacheze Kitimu kufikia kiwango chao.”
Van Gaal aliliona hilo kwenye Mechi na Swansea walipokuwa nyuma 1-0 wakati wa Haftaimu na kumtoa Chicharito na kumwingiza Nani na Mfumo kubadilika kuwa 4-2-3-1 ambao Man United wameuzoea.
Baada ya hilo uhai ulirudi na Man United kusawazisha lakini udhaifu wa Difensi, hasa kumtumia Ashley Young kama Fulbeki, kuliwafungisha.
Hayo yote yananyoosha kidole kwa Man United kuhitaji Wachezaji wapya haraka hasa Masentahafu na Viungo.
Nae Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes, alietimuliwa Mwezi Januari baada ya Miezi 10 tu, akiongea kwenye TV ambapo alikuwa Mchambuzi, alieleza: “Kila Mtu anajua unahitaji muda. Kuchukua wadhifa kutoka kwa Sir Alex Ferguson kunahitaji upewe muda. Louis van Gaal atahitaji muda kufanya kazi yake. Anahitaji nafasi kuleta mabadiliko na kujenga Timu anayotaka. Kilichotokea Leo kufungwa na Swansea kilinikuta mimi dhidi ya West Brom, Newcastle na Everton Mwaka Jana. Hivi sasa kila Timu kwenye Ligi Kuu imejiweka sawa na hujipanga vizuri na unahitaji Wachezaji spesho kukusaidia kushinda.”
Ukweli ni kwamba Man United wanahitaji Wachezaji wapya haraka ama ile Timu ya Moyes, ambayo Mashabiki wanataka kuisahau, itaendelea hivyo hivyo ilivyokuwa Msimu uliopita.
MAN UNITED - MECHI ZIJAZO
Agosti 24 1800: Sunderland v Man United
Agosti 26 2200: MK Dons v Man United [Capital One Cup]
Agosti 30 1445: Burnley v Man United
Septemba 14 1800: Man United v QPR
Septemba 21 1530: Leicester v Man United
Septemba 27 1700: Man United v West Ham
Oktoba 5 1400: Man United v Everton
Oktoba 20 2200: West Brom v Man United
Oktoba 26 1900: Man United v Chelsea

No comments:
Post a Comment