Masihara: Prince Charles na Camilla wakiongea na wachezaji wa mchezo wa badminton wa Wales alipotembelea Emirates
Arena na Chris Hoy Velodrome mjini Glasgow
|
Malkia
kiongozi wa nchi za Jumuiya ya madola anatazamiwa kuhudhuria sherehe
akiwa na Duke wa Edinburgh kwa ufunguzi rasmi wa tukio hilo kubwa kabisa
kwa mwaka huu wa 2014.
Maandalizi
ya mwisho: Celtic Park unazidi kupendeza kuelekea kwenye ufunguzi wa
michezo ya Madola ambayo imeelezewa kuwa itakuwa ni babukubwa.
Uso
kwa uso: Mashabiki wa mataifa mbalimbali wakiungana kwa pamoja Celtic
Park kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya 20 ya Madola 2014.
Mashabiki:
Kikundi cha ushangiliaji cha England wakiwa katika morali ndani ya
uwanja wa Celtic wenye uwezo wa kuchukua watu 40,000 kwa mara moja kabla
ya ufunguzi wa Madola.
Mashabiki wa Scotland wakiwa na kofia na skafu ndani ya Celtic Park
Prince
Charles akitaniana na wachezaji wa Jamaican wa jumuiya ya Madola wa
mchezo wa ngumi alipotembelea Emirates Arena na Chris Hoy Velodrome
Ni maandalizi tu na hali ya kusisimua katika mji wa Glasgow wakati wakati wa utafutaji wa tiketi
MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA YAFUNGULIWA RASMI HII LEO
Michuano ya jumuia ya Madola kwa mwaka 2014, imefunguliwa rasmi hii leo jijini Glasgow nchini Scotland huku mataifa 71 yakitarajiwa kushindana katika michezo 17 tofauti, ambayo itaanza kutimua vumbi lake kesho.
Tayari waziri mkuu wa nchini Scotland, Alex Salmond ameshathibitisha
kukamilika kwa maandalizi ya michuano hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu
kubwa na wadau wa michezo duniani kote, huku kila nchi ikiamini wawakilishi wao
wataibuka na medali ima za dhahabu, shaba ama fedha.
Salmond amewataka wachezaji kutoka kila kona ya dunia
kujihisi wapo nyumbani na washiriki michuano hiyo kwa amani ambayo itafikia
tamati August 3.
Hata hivyo kiongozi huyo amewasihi wanamichezo
watakaoshiriki michuano ya Jumuia ya Madola kwa mwaka huu huko mjini Glasgow,
kujiepusha na kadhia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, ili kuepuka
balaa ambalo huenda likawaharibia maisha yao ya baadae katika nyanja ya
kimichezo.
Amesema vipo vinywaji vya kawaida ambavyo vinatumika na
vinaruhusiwa kwa wanamichezo kuvitumia wakati wote, lakini wasithubutu kwenda
nje ya maadili kwa kunywa vinywaji ama dawa zenye chembe chembe za kuongeza
nguvu.
Waziri mkuu wa nchini Scotland, Alex Salmond. |
No comments:
Post a Comment