Bodi
ya ligi kuu nchini Tanzania imesema kuwa ina orodha ndefu ya waamuzi
waliochezesha ligi mwaka jana ambao kimsingi hawatatumika msimu mpya wa
ligi 2014/15.
Akiongea
na mtandao wa Rockersports mtendaji mkuu wa bodi hiyo Silas Mwakibinga
amesema ni kutokana na makosa mbalimbali ya kutafsiri sheria aidha kwa
bahati mbati au kwa makusudi Bodi yake imeonelea ni vema kuwaengua
baadhi ya waamuzi walionekana na makosa mbalimbali msimu uliopita.
pamoja
walipitia ripoti mbalimbali za michezo ya msimu uliopita na
kujiridhisaha juu ya matatizo ya usimamiaji wa waamuzi wa ligi msimu
uliopitana kwamba maamuzi hayo si ya kumkomoa mtu kwani ripoti hizo zipo
ofisini kwake.
Hata
hivyo Mwakibinga aligoma katakata kuwataja waamuzi waliopigwa chini na
Bodi yake kwa kushirikiana na kamati ya ligi kutokana na sababu za
kimaadili huku akiahidi muda ukifika waamuzi hao wataanikwa hadharani.
Aidha
amesema kuna baadhi ya michezo wamelazimika kupitia upya mikanda ya
video kuangalia matukio ya maamuzi ya wamuzi viwanjani.
Ligi kuu ya Soka nchini msumu mpya 2014/15 inatarajia kuanza Septemba 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment