KAMPUNI
kubwa ya vifaa vya michezo ya Nike ya Marekani inatarajiwa kutoongeza
mkataba mwingine wa kuitengenezea jezi timu ya Manchester United
kutokana na gharama za mkataba mpya. Nike wamekuwa wakitengeneza jezi
maarufu za United toka mwaka 2002 na mkataba wao unatarajiwa kumalizika
mwakani. Kuondoka kwa Nike kunatarajiwa kutengeneza njia kwa kampuni
nyingine ya vifaa vya michezo ya Ujerumani Adidas kuingia mkataba mpya
na klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. United
imetengeneza kiasi cha paundi milioni 38 katika mkataba walioingia na
Nike kwa mwaka 2012-2013, yakiwemo magwanyo ya faida kutokana na mauzo
ya bidhaa zake zenye nembo hiyo duniani. Vyombo vya habari vimeripoti
kuwa United sasa wanataka mkataba mpya ambao utakuwa thamani ya paundi
milioni 60, kiasi ambacho Nike hawako tayari kukilipa.Jezi mpya ya Man United kwa ajili ya msimu mpya 2014/15 Nyumbani
No comments:
Post a Comment