Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 14, 2014

WORLD CUP 2014: SPAIN 1 vs NETHERLANDS 5, VAN PERSIE, DE VIRJ NA ARJEN ROBBEN WALIPA KISASI KWA SPAIN!!!

Kipindi cha pili dakika za mwishoni dakika ya 80 Arjen Robben amewakaanga mabeki na kuwafunga pamoja na kipa wao Spain baada ya kuwazidi mbio na kuachia shuti kali lililofanya mabao kuwa 5-1 dhidi ya Spain ambao ni Mabingwa Watetezi wa Dunia wa Kombe hili.Historia hii...nimetupia 2!!!
Dakika ya 64 tena Stefan de Vrij ameoingozea bao la tatu timu ya Netherlands na kufanya matokeo kuwa 3-1 dhidi Spain. Wesley Sneijder ndie alietoa pande hilo lililozaa bao.
Stefan de Vrij aliyefunga bao la tatu huku van persie akimzonga kipa ili bao lifanikiwe...
De Vrij wa Holland akishangilia baada ya kuichakaza bao la tatu Spain kwa kufanya 3-1 akishangilia kwa raha zake...
Kipindi cha pili dakika ya 53 Arjen Robben alipewa pasi safi na Daley Blind na kufunga bao la pili kwa timu ya Netherlands na kufanya 2-1 dhidi ya Spain.Dakika ya 27 kipindi cha kwanza Xabi Alonso ndie aliyeifungia bao kwa mkwaju wa penati na kuitanguliza mbele Spain kwa bao 1-0 dhidi ya Netherlands. Dakika ya 44 mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha dakika 45 mchezaji matata Van Persie amewatoka mabeki wa Spain na kuruka kwa kichwa maridadi na kuisawazishia bao kwa kufanya 1-1 timu ya Netherlands. Mpaka dakika za kipindi cha kwanza zinamalizika timu zote mbili zilikuwa kwenda kupumzika zikiwa nguvu sawa kwa bao 1-1. Van Persie akitupia.....
VIKOSI:
Spain:
Casillas, Azpilicueta, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Alonso, Xavi, Busquets, Silva, Diego Costa, Iniesta.
Subs: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Torres, Fabregas, Pedro, Mata, Koke, Cazorla, Reina.

Holland: Cillessen, Janmaat, Vlaar, De Vrij, Martins Indi, Blind, De Guzman, Sneijder, De Jong, van Persie, Robben.

Subs: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)

Mchezaji wa Netherlands  Stefan de Vrij  kamwangusha kwenye eneo la Hatari Diego Costa
Xabi Alonso akiifungia bao Spain kwa mkwaju wa penati...
Xabi Alonso wa Spain akishangilia bao lake
Asante baba!!!! Wachezaji wa Spain wakimpongeza Alonso.
Fowadi wa Spain Diego Costa akimwendesha difenda wa Holland Stefan de Vrij LIVE: Spain 1-0 NetherlandsNipishe!!!
Wachezaji wa Spain wakiimba wimbo wao wa Taifa

Wachezaji wa  Holland wakijifua wakiwa wao ni kundi  B kujiweka sawa na kipute na Spain
Wachezaji wa Holland wakijifua vikali
Wachezaji wa Spain nao wakijiweka sawa kuwakabili  Holland
Wachezaji wa Spain wakipasha
Costa kuanza kwenye kipute hiki....
Baada ya muda mfupi ni kipute kuanza...
Jezi za Wachezaji wa  timu ya  Holland

No comments:

Post a Comment