Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni – FIFA Sepp Blatter amesema ilikuwa kosa kuichagua Qatar kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 kwa sababu ya hali ya joto kali nchini humo
Blatter amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Uswisi kuwa, na namnukuu “unajua, kila mmoja hufanya makosa maishani”.
Kiwango
cha wastani cha joto ni nyuzijoto 40 katika miezi ya Juni na Julai,
kipindi ambacho tamasha la kombe la dunia hupangwa kufanyika.
Blatter
amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa dimba hilo la mwaka wa 2022
litaandaliwa katika msimu wa baridi. Wakati huo, kiwango cha joto
hufikia nyuzijoto 25.
Hata
hivyo rais huyo wa FIFA hakuzungumza lolote kuhusu madai ya rushwa
kuhusiana na mchakato wa kupiga kura uliosababisha Qatar kuchaguliwa
kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Hata hivyo amesema kulikuwa na shinikizo kubwa la kisiasa kutoka Ufaransa na Ujerumani.
Wakati huo huo, Brazil inakabiliwa na mtihani wa maandalizi yake ya usalama kwa ajili ya michuano ya dimba la Kombe la Dunia.
Wananchi
wanaokasirishwa na gharama kubwa za kuandaa michuano hiyo wiki hii
walifanya maandamano ya kupinga gharama zinazotumiwa katika maandalizi
ya tamasha hilo pamoja na migomo ya wafanyakazi katika miji kadhaa
mikubwa nchini humo.
Maelfu
ya walimu waliandamana katika mji wa Sao Paulo takriban kwa wiki nane
sasa wakidai kulipwa mishahara mizuri na kuwepo kwa mazingira mazuri ya
kazi.
Migomo
ya kazi inayoendelea kufanywa na walimu hao na polisi na tishio la
kufanyika kwa mgomo wa taifa zima na polisi pia inazusha hofu ya vurugu
ikiwa zimebakia wiki nne tu kabla ya kuanza kwa michuano ya soka Kombe
la Dunia.
Jumla
ya watu 10,000 wamendamana katika mitaa ya mji wa Belo Horizonte,
Barasilia mji mkuu wa Brazil, Manaus, Porto Alegrea, Rio na Sao Paulo.
Katika
mji mkuu wa kibiashara wa Sao Paulo takriban wanachama 5,000 wa Vugugu
la Wafanyakazi wasiokuwa na Makaazi waliwasha matairi ya magari na
kuandamana hadi katika uwanja wa Corinthians Arena ambapo ndipo
patakapofanyika pambano la ufunguzi kati ya Brazil na Coatia hapo Juni
12. Huyu hapa mmoja wa waandamanaji.
Chanzo: DW kiswahili
No comments:
Post a Comment