Tanzania
imeanza Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) inayofanyika nchini Botswana kwa
kutoka sare ya bao 1-1 na Mali kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 15 katika mechi iliyochezwa leo (Mei 22 mwaka huu).
Mechi
hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone ambapo Tanzania ilikuwa ya kwanza
kupata bao dakika ya 52 mfungaji akiwa Amani Ali. Hata hivyo, Mali walifanikiwa
kusawazisha bao hilo dakika ya 61.
Tanzania
itacheza mechi yake ya pili kesho (Mei 23 mwaka huu) kwa kuwakabili wenyeji
Botswana kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 8 kamili mchana kwa saa za Tanzania.
Mechi hizo zinaoneshwa moja kwa moja na kituo cha SuperSport.
No comments:
Post a Comment