Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini leo saa 12:45 kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya
FIFA.
Taifa
Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare
ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya South Africa Airways.
Timu
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli
ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi
yake.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
No comments:
Post a Comment