Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 23, 2014

REFA ANDRE MARRINER AOMBA RADHI KWA KOSA LA KUTOA KADI NYEKUNDU KWA KIERAN GIBBS BADALA YA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN!

REFA Andre Marriner ameomba radhi kwa kumtoa nje Fulbeki wa Arsenal Kieran Gibbs kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge na Arsenal kutandikwa 6-0.
Refa Marriner alitoa Penati baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kutoa nje Shuti la Eden Hazard kwa Mkono lakini akamwonyesha Kadi Nyekundu Kieran Gibbs.
Penati hiyo ya Dakika ya 17 ilizaa Bao la 3 kwa Chelsea na kuwaacha Arsenal wakicheza Mtu 10.

Wakitoa tamko, PGMO [Professional Game Match Officials Limited] ambao ndio husimamia Marefa wa Ligi Kuu England, walisema Matukio ya Refa kukosea kumpa Kadi Mchezaji ni machache na hutokea kwa sababu za Kiufundi.

PGMO imesema Refa Andre Marriner amehuzunishwa na kosa lake kwa kushindwa kumtambua Mchezaji sahihi aliehusika.
Akiongea baada ya Mechi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alidai Refa Marriner hakuliona kabisa tukio zima.
Nae Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, alisema: “Ni tukio ambalo kama una TV, Refa wa Akiba angeweza kutambua sio Gibbs. Bahati mbaya Mchezaji asiehusika alitolewa!”

No comments:

Post a Comment