Stoke City, wakicheza Ugenini Uwanjani Villa Park, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuicharaza Aston Villa Bao 4-1 na kupata ushindi wao wa kwanza wa Ugenini tangu Agosti kwenye Ligi Kuu England.
Villa walitangulia kufunga katika Dakika ya 5 kwa Bao la Christian Benteke alipomalizia krosi ya Fabian Delph lakini Stoke walijibu mapigo na kufunga Bao mbili ndani ya Dakika 4 kwa Bao za Peter Odemwingie na Peter Crouch kwenye Dakika za 22 na 26.
Steven Nzonzi aliipa Stoke Bao la 3 katika Dakika ya na Geoff Cameron kupiga Bao la 4 kwenye Dakika ya 90.Mashabiki wa Aston Villa wakitoka mapema uwanjani baada ya timu yao kutembezewa kichapo cha bao 4-1 kwenye uwanja wao Villa Park usiku huu.Christian Benteke akiadhibiwa na mwamuzi wa mtanange huo baada ya kujiangusha kwenye eneo hatari la penati na kumbwatukia refa huyo Mark Clattenburg.Kocha wa Aston Villa Paul Lambert akipagawa baada ya kuona timu yake ikiendelea kushindiliwa mabao Kwenye Uwanja wao wa Villa Park.2-1Kocha wa Aston Villa Paul Lambert 4-1 na mtanange kumalizikaPeter Crouch kwa furaha baada ya kipute kumalizika!

No comments:
Post a Comment