Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa mpira
wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa
utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Riziki
Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na Samwel
Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume
cha taratibu.
Naye
Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa mchezaji
Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
Kwa
mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo
itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo
walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment